Jumamosi 19 Septemba 2026 - 23:59
Taifa la Iran limesimama dhidi ya vitisho kwa subira, uangalifu na kumtegemea Mwenyezi Mungu

Hawza/ Ayatullah Du'ri Najaf-abadi, akirejea historia ya uhalifu wa madola ya kibeberu, amesema: Taifa la Iran linasimama dhidi ya vitisho kwa subira, uangalifu na kushikamana na Mwenyezi Mungu, na haipaswi kumdharau adui.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Arak, Ayatullah Du'ri Najaf-abadi, mwakilishi wa Walii Faqihi katika Mkoa wa Kati, leo katika darsa yake ya juu ya fiqhi, huku akirejea historia ya vita na uhalifu wa madola ya kibeberu katika maeneo mbalimbali duniani, amesema: Historia imeonesha kwamba madola ya kibeberu, pindi yanapopata mazingira yanayoyaruhusu, hayakwepi kufanya uhalifu wowote ili kufikia malengo yao; hivyo, haipaswi kumdharau adui, bali ni lazima kwa uangalifu na mshikamano wa kitaifa kulinda nchi na maslahi ya wananchi.

Ayatullah Du'ri Najaf-abadi amesisitiza kwamba: Iran ni ardhi ya Ahlul-Bayt (as), ardhi ya Imam Ridha (as), na ni nchi yenye historia na utambulisho wa kina wa Kiislamu na kihistoria, hivyo haiwezi kulinganishwa na nchi nyingine, taifa la Iran, katika vipindi mbalimbali, limeonesha kwamba linasimama imara mbele ya vitisho na shinikizo.

Ameendelea kusema: Taifa la Iran, vikosi vya ulinzi na usalama, wanazuoni na nguvu zote za waumini na wanamapinduzi, wanapaswa kudumisha umakini wao, maadui wana malengo na misukumo mbalimbali, na haipaswi kuangalia tu sura ya nje ya matukio; bali ni lazima kufuatilia masuala kwa umakini na busara.

Mwakilishi wa Walii Faqihi katika Mkoa wa Kati, huku akisisitiza umuhimu wa kuhifadhi umoja na mshikamano wa kitaifa, amesema: Ikiwa hakutakuwa na uangalifu na maandalizi yanayohitajika, adui anaweza kusababisha madhara; hivyo, sote tunapaswa kushiriki katika kuilinda nchi, maslahi ya kitaifa na maslahi ya umma, na tusiruhusu njama zinazopangwa kwa lengo la kuigawa na kuidhoofisha Iran zifanikiwe.

Ameongeza kusema: Leo pia tunapaswa kufahamu kwamba matokeo ya subira na ustahimilivu ni ushindi na heshima; hivyo, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, kuhifadhi umoja na kuongeza maandalizi, tunapaswa kuendelea na njia yetu.

Mwakilishi wa Walii Faqihi katika Mkoa wa Kati, katika kuendelea na darsa yake kuhusu masuala ya tauhidi, huku akirejea riwaya zinazohusiana na fadhila ya kushuhudia tauhidi, amesema: Katika riwaya za Ahlul-Bayt (as), imesisitizwa kwamba hakuna jambo lolote linaloweza kulingana na kushuhudia kauli ya “La ilaha illa-llah” kwa upande wa thawabu na thamani; kwa sababu tauhidi ndiyo msingi wa maarifa yote ya Mwenyezi Mungu.

Ameongeza kusema: Mwanadamu anapaswa kufahamu kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Muumba, anaeruzuku na Msimamizi pekee wa ulimwengu, na hakuna yeyote anayeshirikiana au anayelingana naye katika Dhati Yake, Sifa Zake na Matendo Yake. Qur’ani Tukufu inasema:

«لَیسَ کَمِثلِهِ شَیءٌ» na «لَم یَلِد وَلَم یُولَد، وَلَم یَکُن لَهُ کُفُوًا أَحَدٌ».

Ayatullah Du'ri Najaf-abadi, huku akielezea kwamba kumjua Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa daraja za juu zaidi za maarifa, amesema: Tauhidi, Utume, Uimamu na kutekeleza faradhi za Mwenyezi Mungu ni mkusanyiko uliounganishwa katika njia ya imani na kumwabudu Mwenyezi Mungu, na mwanadamu mwenye imani anapaswa kuyafikisha maarifa haya katika hatua ya utekelezaji katika maisha yake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha